AFISA UGAVI , - Boimanda Morden Construction Co Ltd

Tags

.AFISA UGAVI ,
a. Sifa

 • Awe na shahada au stashahada ya juu katika fani ya manunuzi na ugavi (materials management) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali 
 • Awe na cheti cha CPSP na awe amesajiliwa na PSPTB na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili 
 • Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45 
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta (Accounting packages) 
 • Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili 

b. Majukumu

 • Atatakiwa kutambua mahitaji yabidhaa na huduma mbalimbali za kampuni na kufanya manunuzi kwa wakati muafaka na kwa gharama nafuu kwa kuzingatia sheria ya manunuzi na kanuni zake 
 • Kuwashauri viongozi wa kampuni kuhusu kanuni na taratibu sahihi za kufuata wakati wa kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma kwa ajili ya kampuni 
 • Kwa kusaidiana na viongozi wa kampuni kuweka kumbukumbu ya vifaa vilivyo chakaa, ambavyo havijachakaa na thamani yake 
 • Kuandaa makabrasha ya tenda, na kupokea na kuwasilisha tenda 
 • Kuhakikisha nyaraka zote za ununuzi na uuzaji zinapatikana na kujazwa vizuri kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi 
 • Kuhakikisha kwamba nyaraka zote za ununuzi na uuzaji zinatunzwa vizuri kwa ajili ya kumbukumbu pale zinapohitajika 
 • Atafanya kazi nyingine zozote kwa maelekezo ya manejimenti 


Mwisho wa kupokea maombi ya kazi hizi ni Desemba 31,2016.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa:
Mkurugenzi Mkuu,
Boimanda Modern Construction Company Ltd,
S.L.P 1491,
Iringa.


EmoticonEmoticon