MENEJA (Nafasi Mbili) - Boimanda Morden Construction

Tags

a. Sifa

 • Awe tayari kufanya kazi hiyo katika kituo cha Njombe, Iringa au mahali pengine atakapopangiwa na mwajiri 
 • Awe na shahada katika fani ya Uongozi, Utawala au Rasilimali Watu pamoja na elimu ya Biashara na Fedha 
 • Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45, mwenye uzoefu wa kazi wa zaidi ya miaka miwili katika taasisi inayotambulika 
 • Awe ni mbunifu, mpana katika uelewa wa masuala ya utawala na biashara, mchapa kazi na anayeweza kujisimamia 
 • Awe na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu za uendeshaji wa makampuni 
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta (Accounting packages) 
 • Awe na uwezo wa usuluhishi (reconciliation attitude) 

b. Majukumu

 • Kumsaidia Mkurugenzi Mkuu wa kampuni kutekeleza majukumu ya kila siku ya kampuni 
 • Kumshauri Mkurugenzi Mkuu kuhusu masuala yote yanayohusu wafanyakazi kwa upande wa utendaji kazi, maslahi na mahusiano kazini 
 • Kusimamia na kuongoza shughuli zote za kampuni na kuhakikisha zinakwenda na kuendeshwa ipasavyo 
 • Kuendeleza na kutekeleza mipango yote ya kampuni kwa kushirikiana na idara zake zote 
 • Kutoa msaada wa kiutawala kwa kazi zote za kampuni na kuchukua hatua sahihi za kuboresha utendaji wa jumla wa kampuni 
 • Kulinda mikataba na kuslmarnia mahusiano baina ya kampuni na wateja; na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya watumishi wengine wote 
 • Kuwasiliana na washauri na wakandarasi walioteuliwa na kampuni 
 • Kuwasiliana na serikali na mamlaka zingine za kisheria 
 • Kuandaa mipango kazi, ratiba za miradi, makadirio ya matumizi ya rasilimali na ripoti za utekelezaji wa miradi 
 • Kufanya mikutano ya mradi, uchambuzi na ufuatiliaji 
 • Kuwasiliana na vyombo na taasisi za fedha kuhusu usalama na usahihi Wij rekodi za fedha za kampuni 
 • Atakuwa msemaji wa kampuni akimsaidia Mkurugenzi Mkuu 
 • Atawajibika kwa Mkurugenzi Mkuu na kufanya kazi yoyote ya kampuni kwa maelekezo ya kiongozi huyo 


Mwisho wa kupokea maombi ya kazi hizi ni Desemba 31,2016.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa:
Mkurugenzi Mkuu,
Boimanda Modern Construction Company Ltd,
S.L.P 1491,
Iringa.


EmoticonEmoticon