Mwenyekiti wa kamati ya TEITI - Wizara ya nashati na madini

Tags

Kifungu 7(2} cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika
Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia, Mwaka 2015 

Utangulizi 
Utekelezaji wa shughuli za Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative(TEITI)zinasimamiwa na Kamati ya TEITI yenye wajumbe kumi na tano (15) kutoka makundi matatu:- Asasi za kiraia; Kampuni na Serikalini. Kila kundi linawakilishwa na wajumbe watano ambao uteuzi wao hufanywa kutoka katika makundi husika. Sheria tajwa hapo juu, imewekautaratibu wa katika Kifungu cha 7 wa kumpata Mwenyekiti.

Majukumu ya Kamati TEITI 
Majukumu ya Kamati ni kuhamasisha Serikali kuweka mifumo ya uwazi katika usimamizi warasilimali za madini, mafuta na gesi asilia ili kuboresha mapato na manufaa yanayotokana na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa rasilimali hizo nchini. Mazingira ya uwazi yanayolengwa ili kuwa na manufaa ya rasilimali husika ni katika:
iUtoaji wa leseni na mikataba ya uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia;
ii) Usimamizi katika uwekezaji na uendeshaji;
iii) Ukusanyaji wa mapato; na
iv) Mgawanyo wa mapato na matumizi.

Kufuatia kwisha kwa muda wa Mwenyekiti aliyepo sasa, Kamati ya Uteuzi (Nomination Committee)
inakaribisha maombi kutoka kwa wananchi wenye sifa:-

1. Awe Mtanzania aliye na rekodi ya utendaji uliotukuka;
2. Awe na uelewa na ufahamu mzuri juu ya sekta za Madini, Gesi asilia na Mafuta; na
3. Awe mtu anayeweza kujenga mahusiano ya kikazi na kampuni zilizo katika sekta hii, asasi za
kiraia na Serikali.

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni Desemba 20, 2016; na yatumwe kwa anuani ifuatayo:

Katibu Mkuu, 
Wizara ya Nishati na Madini, 
5 Mtaa wa Samora Machel, 
S.L.P. 2000, 
114724 Oar es Salaam. 
TANZANIA. 
baruapepe: info@teiti.or.tz


EmoticonEmoticon