TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

September 28, 2025 Morogoro

Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba imepata mradi wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi na Urejeshaji wa Uoto katika Mandhari (FOLUR) unaofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) chini ya usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba anatangaza nafasi za ajira za mkataba kwa wananchi wote raia wa Tanzania wenye sifa zifuatazo:


1.0 AFISA UGANI (FIELD EXTENSION OFFICER) – NAFASI 2

1.1 Sifa za Mwombaji

  • Awe na elimu ya Kidato cha Nne au Sita na Shahada (Bachelor’s degree) katika moja ya fani zifuatazo: Kilimo, Maliasili, Ardhi, Mazingira, Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Jamii.
  • Awe na uzoefu wa angalau miaka mitatu (3) katika kupanga na kutekeleza miradi, kuhamasisha na kushirikisha jamii ndani ya Tanzania.
  • Mwenye uzoefu katika miradi ya usimamizi wa maliasili inayotekelezwa na NGOs au Serikali atapewa kipaumbele.
  • Awe na uzoefu wa masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake.
  • Awe na ujuzi wa uongozi, mawasiliano, uwezeshaji na ushirikishaji wadau.
  • Awe na uzoefu wa kushirikiana na viongozi wa kimila, jamii zilizotengwa na timu za kisekta pamoja na maofisa wa Serikali.
  • Awe na ujuzi wa mahusiano binafsi na uwezo wa kuendeleza ushirikiano na wadau wa ngazi ya Wilaya na Jamii.
  • Awe na ufasaha wa kuzungumza na kuandika Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na leseni halali ya udereva na uwezo wa kuendesha pikipiki.

1.2 Kazi na Majukumu

  • Kuratibu mikutano na semina kwa jamii na wadau.
  • Kutekeleza jitihada za kuimarisha jamii kupitia matumizi endelevu ya rasilimali za misitu, maji na ardhi.
  • Kushirikiana na jamii, viongozi wa kimila, Wilaya, Mkoa na Idara za Serikali katika utekelezaji wa shughuli za mradi.
  • Kufanya kazi na Mratibu wa Kongani kuandaa mbinu na mipango ya utekelezaji wa mradi.
  • Kushirikiana na maafisa ugani na washirika kujenga uelewa wa hatua na mahitaji ya mradi.
  • Kurekodi taarifa za shughuli na kushirikiana katika maandalizi ya taarifa za maendeleo ya mradi.
  • Kutoa taarifa kwa ajili ya mfumo wa matokeo na ufuatiliaji wa mpango kazi wa mradi.
  • Kushiriki katika maandalizi ya mpango kazi na warsha za tathmini za mwaka.
  • Kuwezesha msaada wa vifaa na ushauri wa kitaalam katika usimamizi na tathmini ya mradi.
  • Kushughulikia na kuwasilisha malalamiko kutoka kwa jamii.
  • Kufanya kazi nyingine zitakazopangwa na Mratibu wa Kongani.

1.3 Ngazi ya Mshahara

Kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na wasimamizi wa mradi.

1.4 Masharti ya Ajira

Ajira hii ni ya mkataba wa mwaka mmoja (1) unaoweza kuhuishwa hadi miaka minne (4).


2.0 Mambo Muhimu ya Kuzingatia kwa Mwombaji

  • Awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 – 45.
  • Aambatanishe cheti cha kuzaliwa.
  • Awasilishe wasifu binafsi (CV).
  • Aandike barua ya maombi kwa mkono.
  • Aambatanishe nakala ya kitambulisho cha uraia au Namba ya NIDA.
  • Awasilishe nakala za vyeti vya taaluma, kidato cha nne, au kidato cha nne na sita, cheti cha kuzaliwa na picha mbili (passport size).
  • Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na TCU/NACTE na waambatishe barua ya ulinganishi.
  • “Testimonials, Provisional Result, Statement of Result” na Result Slip havitakubaliwa.
  • Taarifa au sifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10 Oktoba, 2025 saa 9:30 Alasiri.


3.0 Namna ya Kutuma Maombi

Barua za maombi ziambatane na:

  • Wasifu binafsi (CV).
  • Nakala za vyeti vya elimu na ujuzi.
  • Cheti cha kuzaliwa.
  • Picha mbili (2) za passport size.

Maombi yatumwe kwa anwani ifuatayo:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba,
S.L.P. 263,
IFAKARA.